Afleveringen
-
Muziki wa HIP HOP nchini Tanzania umefifia kutokana na ugumu wa kufanya Muziki huo,Msanii PMawenge anasimulia hatua za kuchukua kuurejesha sokoni katika Makala ya Nyumba ya Sanaa.
-
Sanaa ya ushairi inawavutia zaidi watu wanaotamani kujua utamu na upekee wa lugha adhimu ya Kiswahili, Chuo kikuu cha Dar es salaam kimewatambua na kuwapa fursa vijana waliosomea fani ya sanaa, kubobea katika kughani Mashairi.
Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa akizungumza na Msanii Michael James maarufu Michael.
-
Zijn er afleveringen die ontbreken?
-
Mwandishi wetu Steven Mumbi amezungumza na kundi la wasani la viongozi generation.
-
Muziki wa kizazi kipya umewawezesha vijana nchini Tanzania kujikwamua kimaisha kwa kujipatia kipato kupitia Sanaa hiyo,Katika Makala haya Steven Mumbi anazungumza na Hussein Mussa Shundi Maarufu Rucky.
-
Msanii wa Bongo Fleva, Baraka the Prince anauona muziki ni maisha, jambo linalomfanya afikirie zaidi namna mashabiki wake wataishi na kazi zake, Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa akizungumza na Msanii huyo.
-
The Mafiki ni kundi la Muziki lililovuma kwa vionjo vya Muziki wa sasa, sasa wamekuja upya mara baada ya kusambaratika, Ungana na Steven Mumbi akizungumza na wasanii wa kundi hilo.
-
Mapinduzi ya Muziki wa Taarab yanajidhihirisha katika tenzi za wasanii wa Muziki huu kutoka tungo za Majigambo na sasa tungo za kuburudisha, Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa akizungumza na Jike la Chui.
-
Zumbukuku ni miongoni mwa nyimbo zilizofanya vizuri katika muziki wa taarab, hii inashehenezwa na sauti ya kipekee ya kiume inayosikika katika muziki huo, Ally Star ndie aliyeimba wimbo huo; Ungana na Steven Mumbi katika makala ya Nyumba ya Sanaa akizungumza na Ally Star kuhusu namna nyimbo hizo zilivyotia fora.
-
Makala ya nyumba ya sanaa wiki hii imepiga kambi mjini Goma huko mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ambako mwanzoni mwa mwezi mei mwandishi wetu Ruben Lukumbuka alikutana na msanii Ogisha Matale ambapo katika shughuli zake zake amekuwa akijaribu kuhimiza amani nchini, hususan eneo lake lenye kushuhudia mapigano ya mara kwa mara.
-
Nyota Tiger ni mzaliwa wa jijini Mwanza nchini Tanzania alilazimika kusafiri mpaka maeneo ya kusini mwa Afrika kukwepa adha za wazazi kumnyima fursa ya kufanya muziki. Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa.
-
Katika makala ya nyumba ya sanaa wiki hii mwandishi wetu Ruben Lukumbuka ambaye hivi karibuni alitembelea mashariki mwa DRC ambako alikutana na Olivier wabahavu, msanii maarufu sana kufuatia nyimbo zake anazoimba katika lugha ya kihavu na kishi huko Kivu kusini na kaskazini, amezungumzia mchango wa sanaa ya muziki wa kiasili katika usuluhishi wa migogoro ya kivita mashariki mwa DR Congo.
-
Muziki wa Singeli ni Miongoni mwa Muziki unaokua kwa kasi nchini Tanzania na nchi za Afrika,Wasanii wa Muziki huo wanapambana kuukuza Kimataifa, Man Fongo ni Miongoni mwa Wasanii Pendwa wa Muziki huo,Ungana na Steven Mumbi anazungumza na Msanii huyo.
-
Katika Makala ya Wiki hii, Steven Mumbi amezungumza naye Jilema Ng'wana Shija msani wa muziki wa asili kutoka nchini Tanzania.
-
Karibu katika makala ya Nyumba ya sanaa nami Steven Mumbi, hii leo Msanii Tourna Boy wa kizazi kipya kutoka mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo akielezea kuhusu juhudi za vijana wasanii kuchangia katika juhudi za kurejesha amani ya mashariki mwa nchi hiyo, katika mazungumzo na mwenzangu Ruben Lukumbuka alipotembelea eneo la Goma mwanzoni mwa mwezi mei mwaka huu 2024
-
Kwenye Makala ya wiki hii Stephen Mumbi anazungumza na msani Abdul Sykes kutoka Mbagala Tanzania.
-
Makala ya Nyumba ya sanaa wiki hii inamuangazia msanii wa muziki wa regae Mack El Sambo ambaye kwa zaidi ya miaka ishirini amekuwa akihimiza amani katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, hususan kwenye mji wa Goma katika mkowa wa Kivu Kaskazini. Ungana na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka ambaye hivi karibuni alitembelea mji wa Goma na kukutana na mwanamziki huyu..
-
Katika Nyumba ya sanaa wiki hii Steaven Mumbi akishirikiana na Ruben Lukumbuka ambaye wiki iliyopita alitembelea mji wa Goma ulioko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambako alikutana na mbunifu wa sanaa mbalimbali ikiwemo ubunifu wa kutengeneza viatu bwana Christian Bazika anayetengeneza bidhaa za ngozi mashariki mwa nchi hiyo.
-
Asha Jumbe maarufu White Maria ni Muigizaji aliyejizolea umaarufu akiwa na umri wa Miaka nane tu, sasa ni mtu Mzima aja kivingine kufanya sanaa ya Fimalu za kiswahili,Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa akizungumzia safari yake ya Uigizaji.
- Laat meer zien