Afgespeeld
-
Karibu katika episode yetu ya 83 ya KijiweNongwa. Tunazungumzia nyimbo mpya toka kwa Marioo, Harmonize na Nandy. Show ya #BongoFlevaHonors ya LadyJaydee, kulinganishwa na Zuchu na umuhimu wa waandishi wa nyimbo. Karibu kutusikiliza.
-
Bado kiwanda cha Bongo Fleva kinaendelea kukumbuka mchango mkubwa wa vijana walioiwakilisha Dodoma mwanzoni mwa mwaka 2001 kupitia ngoma zao kadhaa ambazo zinachezwa na kusikilizwa mpaka hivi sasa.
Wanaitwa Chemba Squad, ambapo ndani yake majina kama Noorah aka Baba stylz, Dark Master, Albert Mangwea na Mez B wa area C yalitajwa kuunda kundi hilo.
Ngoma kama Ice Cream, Ghetto langu na Kama Vipi zinatajwa kama ngoma bora za muda wote kutoka kwa wakali hao ambapo hivi sasa wamebaki wawili tu (Noorah yupo zake Shy Town na Dark Master akiwa Dar es salaam) huku bahati mbaya Ngwea na Mez B wakiwa ni marehemu (RIP).
Leo tunakusogezea historia kamili na mengi usiyoyajua kuhusu Dark Master aka MwanaChemba.
-
Tunazungumzia Komasava Rmx pamoja na kesi ya Ditto na Soggy. Tusikilize.
-
Karibu kwenye episode yetu ya 76 ya KijiweNongwa leo tunazungumzia nyimbo mpya kutoka kwa Rayvanny, Harmonize na Dizasta. Tunaicheki pia album ya BIEN Alusa Why are you topless (Deluxe). Kwa kumalizia tunaangazia Record labels na wasanii. Nini wajibu wa wasanii wetu kwa Record Labels hizi. Tuna imani utaifurahia episode hii.
-
Je, Unamfahamu producer ambaye, dare I say it, bila yeye labda kwaya au bendi yako maarufu usingeisikia kama ulivyoisikia? Producer ambaye amefanya zaidi ya 80% ya production ya mziki wote wa bendi na kwaya Tanzania kwa miaka 30. Marlon Linje, bonge la mshika dau, leo yupo nawe mezani, karibu.